Fonolojia ya Nomino na Vitenzi katika Kimochi

Authors

  • Clarah Nelson Moshi Shule ya sekondari ya Kiboriloni - Moshi
  • Joseph Hokororo Ismail Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto

Abstract

Makala haya yamelenga katika kufafanua vipengele anuwai vya fonolojia vipande sauti vya lugha ya Kimochi. Miongoni mwa vipengele vya kifonolojia vilivyoangaziwa ni irabu, konsonanti, muundo wa silabi, na michakato ya kifonolojia kwa kutumia nadharia ya vipande sauti Huru, iliyoasisiwa na Chomsky na Halle (1968). Data zilizotumika zimekusanywa uwandani katika vijiji viwili vya Mori na Mbokomu vilivyo katika wilaya ya Moshi vijijini, mkoa wa Kilimanjaro. Kama ilivyo katika lugha nyingi za Kibantu, imeonekana kwamba Kimochi kina jumla ya irabu tano (5) na konsonanti thelathini na moja (31) na kwamba michakato mbalimbali inayojitokeza katika Kimochi ni majumui. Hivyo makala haya yatasaidia kwa wanaisimu linganishi kuona mfanano wa vipengele vilivyoshughulikiwa humu na vile vinavyojitokeza katika lugha nyingine za kibantu.

Author Biographies

Clarah Nelson Moshi, Shule ya sekondari ya Kiboriloni - Moshi

Mwalimu

Joseph Hokororo Ismail, Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto

Mwalimu

Downloads

Published

2023-03-27

How to Cite

Moshi, C. N., & Ismail, J. H. (2023). Fonolojia ya Nomino na Vitenzi katika Kimochi. Mulika Journal, 41(2). Retrieved from http://elearning.ucc.co.tz/index.php/mj/article/view/5671

Issue

Section

Articles